Mpanda FM

Mwese kung’arishwa na umeme ifikapo Disemba

14 October 2023, 10:52 am

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akizungumza na wananchi katika Studio za Mpanda Radio Fm

Tanganyika

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema hadi kufikia Disemba 31,2023 wananchi wa vijiji katika kata ya Mwese watakuwa wamefikiwa na huduma ya umeme.

Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Kumekucha Tanzania baada ya wananchi wa eneo hilo kuuliza swali kutaka kujua mustakabali juu ya huduma ya umeme kufika kijijini hapo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Hoza

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanganyika ameendelea kuwataka wananchi hao kuendelea kuwa na subra huku akisema serikali imetenga bajeti kwa ajili ya kufikisha umeme katika vijiji hivyo hadi kufikia desemba 31.

Sauti ya Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika