Mpanda FM

Uelewa mdogo juu ya kansa ya matiti kwa wananchi Katavi

1 October 2023, 6:26 pm

Picha na Mtandao

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuelewa sababu zinazo sababisha   tatizo la kansa ya matiti

Katavi

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuelewa sababu zinazosababisha tatizo la kansa ya matiti kwa wanawake ili kupata ufumbuzi wa haraka kipindi dalili zinapojitokeza.

Mganga Mkuu manispaa ya Mpanda Paulo Swakala akizungumza na Mpanda radio fm  Ameainisha sababu zinazo pelekea wanawake kupata kansa ya matiti  ikiwemo  sababu za umri  huku akizungumza kuhusu mtahasi wa kuwa kila mwanamke anaweza kupata saratani ya matiti.

Katika hatua nyingine wakizungumza na Mpanda Radio fm kuhusu  juu ya kansa ya matiti wananchi wa manispaa ya Mpanda   Wameeleza  uelewa kuhusu namna wanavyoifahamu saratani ya Matiti.