Mpanda na kampeni dhidi ya wazazi wanaoshindwa kupeleka watoto shule
28 September 2023, 7:17 am
Mansipaa ya Mapanda yaanzisha kampeni ya kufuatilia wazazi na walezi wanashindwa kuwapeleka Watoto shule
Na John Benjamin – Mpanda
Halmashauri ya mansipaa ya Mapanda mkoani Katavi imeanzisha kampeni ya kufuatilia na kuhakikisha inawachukulia hatua wazazi na walezi ambao wanashindwa kuwapeleka Watoto shule.
Ugumu wa Maisha,kutokutenga muda wa kufuatilia mwenendo wa mtoto shuleni,malezi ya upande mmoja ndiyo sababu ambazo zinapelekea kuwepo kwa wimbi la utoro kwa Watoto shuleni
Afisa elimu shule za msingi halmashauri ya mansipaa ya Mpanda Godfrey Kalulu akizungumza na Mpanda redio fm amesema kuwa kila mzazi au mlezi anawajibu kuhakikisha anamfuatilia mtoto na anahudhuria masomo yake ipasavyo
Baadhi ya wananchi mkoani hapa wamesema kuwa ugumu wa Maisha,kutokutenga muda wa kufuatilia mwenendo wa mtoto shuleni,malezi ya upande mmoja ndiyo sababu ambazo zinapelekea kuwepo kwa wimbi la utoro kwa Watoto shuleni ambapo wamewaomba wazazi kuhakikisha wanafatilia mahudhurio ya mtoto shuleni.
Kupitia takwimu zilizotolewa na Wizara ya Tamisemi imetaja mkoa wa Katavi jumla ya wanafunzi 9474 wameacha shule kwa mwaka 2022.