Shughuli za utafutaji zinavyochangia utelekezaji wa familia
28 September 2023, 12:09 am
Wazazi na walezi mkoani Katavi wameaswa kuachana na tabia ya kusafiri kwa lengo la kufanya shughuli za utafutaji na kutelekeza familia
Na William Liwali – Katavi
Wazazi na walezi mkoani Katavi wameaswa kuachana na tabia ya kusafiri kwa lengo la kufanya shughuli za utafutaji na kutelekeza familia hali inayosababisha watoto wengi kujiingiza katika vishawishi na kuharibikiwa kimaisha.
Changamoto wanazopitiawatoto hao ni pamoja na kukosa muda wa masomo lakini pia kushindwa kuhimili baadhi ya vishawishi kutoka kwa watu wanaowazunguka kulingana na hali ngumu ya uchumi wa familia.
Wito huo umetolewa na inspekta Kelvin Fuime kutoka kitengo cha polisi jamii na dawati la jinsia na watoto mkoa wa Katavi na Kuainisha madhara yanayoweza kujitokeza endapo watoto wataishi wenyewe bila uangalizi wa wazazi.
Nao baadhi ya watoto wameeleza changamoto wanazopitia ikiwa ni pamoja na kukosa muda wa masomo lakini pia kushindwa kuhimili baadhi ya vishawishi kutoka kwa watu wanaowazunguka kulingana na hali ngumu ya uchumi wa familia.
Kwa upande wa baadhi ya wazazi wamelitazama swala hilo katika mtazamo hasi na kusema kuwa yapo madhara ikiwemo kushindwa kujisimamia katika misingi bora na kuangukia katika makundi yasiyofaa kutokana na uhuru walionao kwa wakati huo.