Manispaa ya Mpanda yapokea dozi 500 kuelekea siku ya kichaa cha mbwa
26 September 2023, 6:03 pm
Kuelekea Maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani Manispaa ya Mpanda imepokea dozi mia tano kwa ajili ya kuchanja ili kukabiliana na kichaa cha Mbwa.
Na Alvero Solomon – Mpanda
Katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani Manispaa ya Mpanda imepokea dozi mia tano kwa ajili ya kuchanja ili kukabiliana na kichaa cha Mbwa.
Wananchi wafike katika ofisi za kata mbalimbali zinazopatikana manispaa ya Mpanda Kuanzia sept 25 mpaka sept 28 kwa ajili ya kupata chanjo hiyo.
Akizungumza na Mpanda radio Fm afisa mifugo na uvuvi Manispaa ya Mpanda Tulinaos Nswila amesema kuwa lengo la kutoa chanjo hiyo katika kuelekea maadhimisho hayo ni kusaidia jamii kuepukana na madhara ya kichaa cha Mbwa.
Aidha Tulinao Amewataka wananchi kufika katika ofisi za kata mbalimbali zinazopatikana manispaa ya Mpanda Kuanzia sept 25 mpaka sept 28 kwa ajili ya kupata chanjo hiyo.
Katika hatuanyingine wakizungumza na Mpanda Radio FM Kuhusu Uelewa wa kichaa cha Mbwa wananchi Manispaa ya Mpanda wamekuwa na uelewa mseto huku baadhi wakiwataka wamiliki wa mbwa kuwapeleka kuchanja ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza kwabinadamu.
Maadhimisho ya kichaa cha mbwa duniani hufanyika Kila mwaka ifikapo September 28.