Mpanda FM

Eden yafutwa machozi kilio cha maji

20 August 2023, 3:06 pm

MPANDA

Wananchi wa mtaa wa Edeni kata ya Misukumilo halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamemshuru Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi kwa kuwapambania haraka kupata huduma ya maji safi na salama.

Hayo yanajiri kufuatia ziara ya Mbunge wa jimbo hilo baada ya kuwatembelea wananchi wa mtaa huo kupaza sauti zao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama ambapo wananchi hao walimnywesha maji ambayo wamekuwa wakitumia ikiwa ni njia mojawapo ya kufikisha ujumbe wa adha wanayoipata.

Hamis Peter Kisole ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mtemi Beda amesema kuwa wanashukuru kwa jitihada za haraka zilizoanza kufanywa za kuchimba kisima ambacho kinakwenda kuwahudumia wananchi wa eneo husika.

Naye Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ameishukuru serikali kwa kuweza kufanyia kazi malalamiko ya wananchi ambayo aliyafikisha huku akiwaomba wananchi kulinda miundombinu ambayo itawezesha kupata huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayamaji