Lugonesi, Kasekese wajengewa uwezo
9 August 2023, 7:03 am
TANGANYIKA
Kamati za shule ya msingi Lugonesi na shule ya msingi Kasekese wilayani Tanganyika mkoani Katavi zimejengewa uwezo wa namna ya kusimamia Rasilimali za shule pamoja na utolewaji wa elimu bora kwa wanafunzi.
Akizungumza katika kikao cha mafunzo hayo afisa elimu awali na msingi wilaya ya Tanganyika mwl Gidion Bunto amesema mafunzo hayo yaliyotolewa yatasaidia usimamizi nzuri wa fedha za serikali pamoja na rasilimali za shule .
Mkurugenzi wa taasisi iliyowezesha mafunzo hayo ya usevya development society( UDESO) Eden Wayimba, kwa ufadhili wa taasisi ya wajibu amesema wako tayari kushirikiana na kamati zingine katika kutoa mafunzo ya namna hiyo ili kuboresha usimamizi wa miundombinu na kuboresha swala la elimu kwa wanafunzi kwa shule za msingi.
Akifunga mafunzo hayo Mthibiti ubora wa shule wilaya ya Tanganyika, Nyasimbo Masegenya amewataka wanakamati hao kuzingatia kile walichojifunza ili kuleta mabadiliko katika shule hizo.