Hati miliki za ardhi zatolewa Tanganyika
24 July 2023, 10:06 am
TANGANYIKA
Taasisi ya Jen Goodall kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Tanganyika chini ya mradi wa uhifadhi wa maliasili Tanzania wamefanya uzinduzi na ugawaji wa hati miliki katika kijiji cha Vikonge halmashauri yaTanganyika.
Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Mkurugenzi Taasisi ya Jen Goodall Dr Kasukura Nyamaka amesema taasisi hiyo imetambua migogoro ambayo wananchi wamekuwa wakikumbana nayo hivo upatikanaji wa Hati hizo utakwenda kumaliza changamoto hizo kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Aidha kwa upande wake mgeni rasmi ambaye ni waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Geofrey Pinda amesema upatikanaji wa hati hizo utakwenda kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imekuwa kikwazo kwa wananchi wengi katika baadhi ya maeneo halmashauri hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi walio kabidhiwa hati hizo wameishukuru taasisi hiyo ya Jen Goodall huku wakisema kupatikana kwa hati hizo itakwenda kumaliza migogoro yote ambayo imekuwa kikwazo baina yao kwa kipindi kirefu.