Mpanda FM
Ajinyonga Katavi kisa ugomvi na mkewe
30 June 2023, 10:29 am
MPANDA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ali Dodoma Shedrack[32] mkazi wa mtaa wa Msasani kata ya Mpanda Hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amekutwa amejinyonga nyumbani kwake huku chanzo cha tukio hilo likisadikika kuwa ni ugomvi kati yake na mkewe.
Akizungumza na Mpanda Radio Fm mama mzazi wa kijana huyo ameelezea tukio hilo na kusema kuwa mwanae hakuwa na tatizo lakini baada ya mke wake kuondoka na kwenda mahali pasipojulikana ndipo mwanae akachukua uamuzi huo.
Kwa upande wake mjumbe wa serikali ya mtaa wa Msasani Patrick Sokola amesema kuwa alipokea taarifa hiyo majira ya saa nane usiku baada ya marehemu huyo kujaribu kujiua mara ya kwanza na kushindikana.