PETS Wapongeza Shirika la UDESO
9 May 2023, 8:20 pm
KATAVI
Wananchi na wanakamati ya PETS wilayani Tanganyika mkoani katavi, wanaoshiriki mafunzo ya ufahamu wa haki, wajibu na majukumu ya wananchi katika usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya pesa zinazotolewa na serikali kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo wamelipongeza shirika la UDESO kwa kuwapa mafunzo hayo.
Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamesema kuwa mafunzo hayo yatawapa uelewa mzuri wa namna ya kufuatilia miradi ya maendeleo katika maeneo yao huku wakiahidi kuwa mabalonzi wazuru kwa wananchi wengine.
Awali akifungua mafunzo, mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali USEVYA DEVELOPMENT SOCIETY (UDESO) Eden Wayimba amesema kuwa ili kuleta chachu ya maendeleo ni mujibu wa kila mwananchi kusimami na kuhakikisha analinda mali za umma kwani mali za umma ni za wana jamii wote.
Halima Kituruma ni msajili msaidizi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wilayani Tanganyika amesema kuwa anasimamia lengo kuu la mafunzo hayo litimie kama ilivyokusudiwa na shirika.