BUSWELU “Tumieni Sheria Kutekeleza Mpango Bora wa Matumizi ya Ardhi Mishamo”
27 April 2023, 8:31 am
TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelo Amewataka Viongozi na Wananchi Mishamo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kufuata sheria zinazotakiwa ili kufuata na kutekeleza Mpango bora wa matumizi ya Ardhi Mishamo.
Akizungumza katika kikao cha wasilisho Mpango bora wa matumizi ya ardhi Mishamo amesema ili kuepusha migogoro ikiwemo ya wakulima na wafugaji inayojitokeza Wananchi na viongozi wanapaswa kutelekeza sheria za ardhi zinavotaka.
Awali afisa mipango Miji Mkoa wa Katavi Ibrahimu Butta akiwasilisha mpango wa matumizi ya ardhi Mishamo Ameainisha lengo la kuandaa mpango huo ni kuepusha migorogoro, kuhifadhi mazingira Mishamo huku Akianisha moja ya changamoto walizozibaini katika Mpango ni matumizi mabaya ya ardhi kwa wakulima Na wafugaji inayopelekea kuathiri matumizi ya ardhi.
Kwa upande wao wananchi wakiwawakilisha wakulima na wafugaji wameshukuru kwa serikali kuja na mpango wa matumizi bora ya ardhi kayika eneo la mishamo utaosaidia kupunguza changamoto zote zilizoonekana.
Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu kikao cha kwanza kufanyika tarehe 3.03.2023 kikiwana lengo la kufanya uhamasishaji kuelekea uandaaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi Mishamo.