Idadi ya Watu Kwenda Kupata Chanjo Yaongezeka
18 April 2023, 8:45 pm
MPANDA
Idadi ya watu wanaojitokeza kwenye vituo vinanyotolea huduma za Chanjo imeongezeka kutokana na hamasa inayotolewa na Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya watu waone umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 na chanjo za aina nyingine .
Mratibu msaidizi wa Chanjo wa Manispaa ya Mpanda Patrick Kumburu Amesema kuwa idadi ya watu wanaojitokeza kwenye vituo vya kutolea chanjo ya Uviko 19 imeongezeka kufatia wananchi kupata uwelewa.
Kumburu amefafanua kuwa vyombo vya habari vimesaidia kuwafanya wananchi watambue umuhimu wa huduma ya chanjo ya UVIKO 19 lakini hata magonjwa mengine ya mlipuko wa janga la surua lililokuwa limeukumba Mkoa wa Katavi .
Meneja wa shirika la Tanzania Youths Behevioral Organization(TAYOBECO) Adinani Mussa amesema kuwa kwa zaidi ya miaka mitatu shirika la INTERNEWS Tanzania limekuwa likitekeleza mradi wa boresha habari unao fadhiliwa na USAID
Lengo la mradi huu ni kuwahamasisha vijana na wanawake umuhimu wa chanjo ya Uviko 19 pamoja na chanjo nyingine mbalimbali ikiwemo chanjo ya surua na kwa makundi mengine mbalimbali wakiwepo na wazee .