Joy FM

DC Kigoma ataka vikundi kurejesha mikopo kwa wakati

3 April 2026, 10:28

Baadhi ya wawakilishi wa vikundi 24 vilivyopokea mikopo ndani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Tryphone Odace

Benki ya CRDB Kigoma imetoa elimu ya fedha kwa vikundi mbalimbali vilivyopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji lengo likiwa ni kuviwezesha vikundi hivyo kufahamu namna ya kutumia mikopo wanayopewa ili iweze kuwanufaisha zaidi.

Na Tryphone Odace

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua amevitaka vikundi vinavyonufaika na mikopo inayotelewa na Halmashauri kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa lengo lililokusudiwa ili waweze kuzalisha na kuweza kurejesha ili vikundi vingine viweze kunufaika na mikopo hiyo.

Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua, Picha na Tryphone Odace

Dkt. Chuachua amesema hayo leo wakati akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo kwa vikundi 24 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu na kuwa lengola serikali ni kuhakikisha mikopo hiyo inawanufaisha watu wote.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua

Aidha amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na benki ya CRDB wataendelea kuvifuatilia vikundi hivyo na kuvipatia elimu ya fedha ili waweze kutambua nama ya kutumia mikopo hiyo vizuri.

Baadhi ya wawakilishi wa vikundi 24 vilivyopokea mikopo ndani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Picha na Tryphone Odace

Naye Mkuu wa Idara ya Maenedeleo ya jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Jabir Majira amesema mikopo ya mikopo hiyo ni kuwasaidia kukuza mitaji yao.

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Maenedeleo ya jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Jabir Majira

Msimamizi wa mikopo ya asilimia kumi kanda ya Magharibi Bi. Editha Nihbagilasoka amesema CRBD imeendelea kushirikiana na serikali kwa lengo la kuhakikisha wanavisimamia vikundi vyote vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambao ndio wanufaika na mikopo hiyo ili waweze kufanya uzalishaji wa mikopo wenye tija.

Sauti ya Bi. Editha Nihbagilasoka
Mkuu wa Idara ya Maenedeleo ya jamii Manispaa ya Kigoma Ujiji Jabir Majira, Picha na Tryphone Odace

Hata hivyo Baaadhi ya wanafaika wameeleza namna elimu ya fedha waliyopata itakavyosaidia kutumia mikopo hiyo ambayo wamepatiwa.