Joy FM
Joy FM
6 March 2026, 11:36

Katika dunia ya leo, ujuzi wa kazi ni muhimu kwa maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla na wengi wanahitaji mafunzo ya vitendo ili waweze kujitegemea na kuchangia katika maendeleo ya jamii ambapo VETA imekuwa na mchango mkubwa katika kuwasaidia vijana kupata na kuongeza ujuzi wa kazi.
Na Timotheo Leonard
Katika jitihada za kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa kujitegemea, Chuo cha ufundi stadi VETA Kigoma kinaendelea kuwa kitovu cha mabadiliko kwa vijana wengi Mkoani Kigoma.
Ndani ya siku 100 za uongozi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, chuo hicho kimefanikiwa kupanua fursa za mafunzo ya ufundi kwa vijana na wanawake.
Chuo cha ufundi Veta Kigoma kimeendelea kuwasaidia vijana mbalimbali ili kufikia ndoto zao ambap taarifa zinaonesha kuwa hadi kufikia Desema 2025, zaidi ya wanafunzi 517 wamejiunga na kozi za muda mrefu katika fani mbalimbali ikiwemo ufundi magari pamoja na ubunifu na ushonaji wa mavazi.

Lakini nyuma ya Takwimu hizo kuna simulizi za maisha ya vijana ambao sasa wanaona matumaini mapya.
Wanafunzi wa fani za ushonaji na tehama nao wanaeleza faraja yao kutokana na mafunzo wanayoyapata kwenye chuo hiki cha Veta.

Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, jitihada zina lengo la kuwajengea uwezo vijana kujiajiri na kuajiriwa huku wakichangia maendeleo ya uchumi wa taifa, kama anavyoeleza Mhandisi Paul Kimenya Mkuu wa chuo cha VETA Kigoma
