Joy FM
Joy FM
15 July 2025, 11:35

Serikali imesema inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji kwa kuhakikisha inaboresha na kupanua uwanja wa ndege Kigoma ili uweze kuwa na hadhi ya kimataifa.
Na Josephine Kiravu
Mradi wa Upanuzi na Uboreshaji wa uwanja wa ndege Kigoma ambapo kukamilika kwake ilipaswa kuwa August mwaka huu imeeleazwa kuwa mpaka Sasa umefikia asilimia 27.5 huku chanzo Cha ucheleweshwaji kikitajwa kuwa ni uwepo wa mvua kubwa zilizonyesha maeneo ya mradi pamoja na mabadiliko ya bei ya vifaa.
Ujenzi huu unatajwa kubadilisha taswira nzima ya uwanja kwa kuupa mwonekano wa kimataifa licha ya kwamba utekelezaji wa mradi umechelewa kukamilika kama anavyoeleza hapa Meneja wakala wa barabara nchini TANROADS Mhandisi Narcis Choma.

Na hapa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro anawatoa hofu wananchi na kwamba mradi utakamilika Kwa wakati na kuwa kichocheo Cha uchumi.
Katika mradi huo wa ujenzi na uboreshaji wa uwanja wa ndega serikali imeweka zaidi ya shilingi bilioni arobaini na sita ili kuhakikisha usafiri wa anga kwa mkoa wa kigoma unakuwa wa kiwango cha kimataifa.