Joy FM
Joy FM
10 July 2025, 12:46

Halmashauri ya Wilaya Kakonko Mkoani Kigoma imetakiwa kuweka mikakati ya kuzalisha mazao ya biashara yenye ushindani ndani na nje ya nchi kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Na Josephine Kiravu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amesisitiza kutengwa kwa maeneo ya uwekezaji pamoja na kuendelea kuzalisha mazao kwa wingi ikiwemo zao la parachichi pamoja na kuyatafutia masoko mazao hayo.
Ni katika mwendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma katika halmashauri zote za wilaya ya Kigoma ambapo hapa anazungumza na watumishi wa uma pamoja na kukagua miradi ya maendelo.
Akiwa Wilayani Kakonko amezungumza na watumishi kubwa akisistiza uzalishaji wa mazao ya biashara pamoja na chakula kwa ajili ya kuvutia wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo nchi jirani ya Burundi.

Ameongeza kuwa ili kukua kiuchumi ni lazima kuongeza kasi kwenye kilimo cha kisasa huku akisistiza pia suala la ulipaji ushuru.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Evance Malasa licha ya kueleza mafanikio ya kiuchumi lakini amesema changamoto iliyopo kwa Sasa ni ubovu wa barabara ya kuwangunisha kibiashara na wananchi kutoka nchi jirani ya Burundi.

Na hapa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Mashimba Ndaki ameeleza mafanikio kwenye ukusanyaji mapato na kusisitiza kufanya vyema zaidi mwaka ujao.
Mkuu wa Mkoa Kigoma akiwa Wilayani Kakonko ametembelea ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa jengo la kuhifadhi miili katika hospitali ya Wilaya na kuagiza jengo hilo lianze kufanya kazi kuanzia august mosi mwaka huu.