Joy FM

Zaidi ya vijana 500 kunufaika na kiwanda cha sukari Kasulu

9 July 2025, 14:57

Muonekano wa miwa iliyopo katika shamba la kiwanda cha sukari kilichopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Kiwanda cha miwa kilichopo Wilayani Kasulu kuwanufaisha vijana na kukuza uchumi.

Na Josephine Kiravu

Mkoa wa Kigoma unaendelea kufanya vizuri kitaifa katika sekta ya uwekezaji ambapo Hadi Sasa wawekezaji wameendelea kuwekeza Kwa kujenga viwanda na kufanya vijana wengi kupata ajira kupitia uwekezaji huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma balozi Simon Sirro akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa ametembelea eneo la uwekezaji Kasulu nakukuta vijana zaidi ya 500 wakiwa wamepata ajira na kuzitaka Halmashauri zingine kutenga maeneo Kwa ajili ya uwekezaji.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma balozi Simon Sirro
Muonekano wa mitambo katika kiwanda cha sukari kilichopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Na hapa amemtaka mwekezaji wa kiwanda hiki Cha sukari kuajiri pia vijana wa Kasulu wenye fani zinazohitajika kiwandani hapo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma balozi Simon Sirro

Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa kiwandani hapo mwekezaji wa kiwanda hicho ameeleza changamoto zinazowakabili huku kubwa ikiwa ni kukosekana Kwa huduma ya umeme wa uhakika.

Hata hivyo Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa tayari Serikali imetenga bajeti Kwa ajili ya kuboresha na kutatua changamoto ya uaptikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika.

Kiwanda hicho Cha sukari kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2027 huku kikitajwa pia kuwa mkombozi Kwa wana Kasulu kwa kutoa ajira Kwa vijana wenye fani zinazohitajika kiwandani hapo.