Joy FM

Watumishi wa umma watakiwa kufanya kazi kwa weledi Kasulu

8 July 2025, 13:10

Wakuu wa taasisi za serikali na binafsi WilayaniKasulu wakiwa katika Mkutano na Mkuu wa Mkoa Kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Watumishi wa umma Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha wanafikisha huduma bora kwa wananchi.

Na Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simoni Sirro amewataka watumishi Wilayani Kasulu kufanya kazi Kwa weledi ili kufanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi.

Balozi Sirro amesema hayo wakati akizungumza na watumishi kutoka idara mbalimbali Wilayani Kasulu ambapo ameweka msisitizo kwa watumishi hao kuimarisha uwajibikaji kazini.

Amesema ili kuinua uchumi wa wananchi ni lazima kuweka mikakati thabiti ikiwemo kutafuta wawekezaji pamoja na vyanzo vya utalii na namna ya kukabiliana na vitendo hivyo.

Viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Kasulu wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa Kigoma, Picha na Josephine Kiravu

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanal Isack Mwakisu amesema mpaka sasa wameendelea kutafuta wawekezaji huku akigusia suala la amani akisema wataendelea kusimamia vyema licha ya kuwa wanapakana na nchi jirani.

Mkuu wa Mkoa ameanza ziara yake ya kikazi ya siku nne ambapo atazungumza na watumishi pamoja na kutembelea miradi ya maendelo katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma