Joy FM

Baba ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumlawiti binti yake

2 July 2025, 16:43

Muonekano wa Nyundo ya mahakamani Picha na Mtandao

Mwanaume mmoja amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kike mwenye miaka sita.

Na Kadislaus Ezekiel

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua amethibitisha mtu mmoja kufungwa kifungo cha maisha jera baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wake  wa kike mwenye umri wa miaka sita, huku akitangaza  vita kwa wanaofanya matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto.

Dkt. Chuachua amesema hayo wakati wa mkutano na viongozi wa dini na wakazi wa Manipaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma katika kongamano la kuombea watoto na taifa lililofanyika katika kanisa la pentekoste mmpt misheni ya gungu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua

Msisitizo ni wazazi, walezi, na viongozi wa dini kutambua wajibu wao katika malezi ya watoto.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua

Makamu Askofu wa kanisa la MMPT Misheni ya Gungu Manispaa ya Kigoma Kigoma Ujiji, Wiliam Stephano anawataka wazazi na walezi kutambua wajibu wao katika malezi.

Sauti ya Makamu Askofu wa kanisa la MMPT Misheni ya Gungu

Kuhakikisha watoto wanakuwa salama, wazazi wakaeleza kuwatunza watoto kwa ukamilifu katika mambo ya imani na kutimiza mahitaji yao.

Sauti ya wazazi na walezi