Joy FM

Uzalishaji wa maziwa kwa wafugaji bado hafifu Kigoma

24 June 2025, 12:05

Wafugaji wakiwa wanaonyesha maziwa wanayozalisha, Picha na Orida Sayon

Wananchi wametakiwa kuzingatia unywaji wa maziwa safi na salama kwa ajili ya afya yao.

Na Orida Sayon

Ukosefu wa elimu kuhusu afya ya mifugo imetajwa kuwa changamoto ya uzalishaji wa mazao ya maziwa katika halimashauri za wilaya za Kigoma, Buhigwe, Uvinza na Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Katika kuadhimisha wiki ya maziwa katika halmashauri ya wilaya za Kigoma,Uvinza, Buhigwe na Manispaa ya Kigoma Ujiji maafisa mifugo kutoka halmashauri hizo wametumia siku hii kueleza taarifa za uzalishaji wa maziwa huku uzalishaji wa maziwa ukionekana hauridhishi kulinganisha na mifugo iliyopo
na changamoto zinazokumba ufugaji.

Aidha afisa mifugo kutoka halmashauri ya Buhigwe Dkt Leonard Godfrey Jeremia amebainisha kuwa utumiaji hafifu wa maziwa katika jamii kupelekea ukosefu wa soko la maziwa na mfugaji kubaki katika hali duni.
Akiwakilisha wakurugenzi wa halmashauri hizo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Kisena Mabuba amesisitiza wafugaji kuzingatia kanuni za ufugaji nakujikita katika ufugaji wa kisasa utakaoongeza uzalishaji ili kutosheleza mahitaji ya watumiaji.

Kwa upande wake, Katibu tawala Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota ameagiza idara zote kuanzisha mashamba darasa ili kutoa elimu ya ufugaji wenye tija akisisitiza wananchi kutumia maziwa ili kujienga na kulinda afya.

Sauti ya Katibu tawala Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota

Wiki ya maziwa huadhimishwa kitaifa kila ifikapo may 28-juni 1mwaka huu iliadhimishwa katika mkoa wa morogoro ikibebwa na kaulimbiu yab “Maziwa salama kwa afya na uchumi endelevu”.

Bango la siku ya unywaji wa maziwa kutoka Wilaya ya Uvinza wakiwa wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika Manispaa ya Kigoma