Joy FM
Joy FM
23 June 2025, 13:20

Serikali Wilayani Kasulu imesema itaendelea kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi vya wenye ulemavu, vijana na wanawake.
Na Emmanuel Kamangu
Halamshauri ya Wilaya ya Kasulu imekabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni 800 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika robo ya tatu na nne ya January hadi june 2024/2025.
Akiwakabidhi hundi hiyo mgeni rasmi wa hafla hiyo, Mbunge wa jimbo la Kasulu vijijini Bw, Augustine Vuma amewasihi wanufaika wa mkopo huo kuzitumia fedha hizo vizuri na kurejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kukopa.
Awali mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilya ya Kasulu Bi, Victoria Moses amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25, zaidi ya fedha takribani billion moja zimetolewa kwa vikundi zaidi ya 80 ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ikilenga kuwakwamua kiuchumi.

Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wamesema wanakila sababu ya kuishukuru Serikali kwa kuwapa mikopo nafuu isiyokuwa na riba jambo litakalowafanya kuwa rahisi kuimalika kiuchumi.
Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilayani Kasulu Bw, Mbelwa Chidebwe amesema mikopo hiyo ni matokeo mazuri ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho katika kuwavusha kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.