Joy FM
Joy FM
13 June 2025, 17:03

Serikali kuendelea kuboresha sera na sheria kuhusu watu wenye ualbino nchini.
Na Kadislaus Ezekiel
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua mahususi kuboresha mifumo ya Kisera na sheria katika kuboresha huduma za watu wenye Ualbino ili kudhibiti ukatili dhidi yao na kuagiza wakuu wa Wilaya kote Nchini, kuhakikisha Jamii ya watu wenye Ualbino inalindwa na kupatiwa huduma zote muhimu kama watu wengine.
Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa, amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kukuza uelewa kuhusu Ualbino, mpango unaolenga watanzania kutambua umuhim wao na kushirikishwa katika masuala ya maendeleo.

Katika maadhimisho hayo, yamehusisha uzinduzi wa APP ya ALBINO MOBILE, inayolenga kusaidia kutambua Ualbino Walipo maeneo yote Nchini na kuweza kusaidiwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Tanzania TASS Godson Mollel, ameomba serikali kuendeela kudhibiti matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino, wakati mkuu wa mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Thobias Andengenye akiahidi kuendelea kuchukua hatua juu ya usalama wa watu wenye Ualbino na ulemavu.