Joy FM

Taasisi za umma zatakiwa kusimamia usafi wa mazingira

4 June 2025, 09:43

Watumishi wa Halmashauri wilaya ya Kasulu wakifanya usafi kituo cha afya Nyakitonto.Picha na Hagai Ruyagila

Wakuu wa Taasisi za Elimu pamoja na idara ya Afya halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia suala la usafi wa mazingira ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafuzi wa mazingira.

Na, Hagai Ruyagila

Usafi wa mazingira ni mbinu za kuzuia upanuzi wa maradhi hasa kwa kudhibiti taka ambazo zinaweza kusababisha magonjwa ya binadamu na  maambukizi kutoka mtu mmmoja kwenda wengine.

Halmashauri ya wilaya ya Kasulu imezindua zoezi la usafi wa mazingira katika kituo cha afya nyakitoto ambapo afisa Mazingira wa Halmashauri ya hiyo Hassan Omary ametoa wito kwa taasisi na wananchi kwa ujumla kuhusu hatari ya utupaji taka ovyo.

Sauti ya afisa Mazingira wa Halmashauri ya hiyo Hassan Omary

Upungufu wa usafi wa mazingira ndiyo sababu kuu ya maradhi duniani kote tumbo la kuharisha nakadhalika hivyo Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii afisa afya halmashauri ya wilaya ya Kasulu Patrick Mihayo anasisitiza usafi wa mazingira katika jamii.

Sauti ya afisa afya halmashauri ya wilaya ya Kasulu Patrick Mihayo

Kaimu Mganga Mfawidhi kituo cha afya Nyakitonto licha ya kutoa shukrani kwa uongozi wa halmashauri na wananchi kufanya usafi katika kituo hicho anaelezea hatua madhubuti za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Sauti ya Kaimu Mganga Mfawidhi kituo cha afya Nyakitonto

Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa takangumu na maji machafu wananchi wa kata ya nyakitonto wanasema uzinduzi wa usafi wa mazingira ni mwanzo mzuri wa kuhamasisha jamii kuwa makini na magonjwa ya mlipuko ambayo chanzo chake ni uchafu.

Sauti ya wananchi wa kata ya Nyakitonto

Uzinduzi wa wiki ya siku ya mazingira duniani imebebwa na kaulimbiu isemayo Mazingira yetu Tanzania ijayo tuwajibike sasa dhibiti matumizi ya plastikiki.