Joy FM
Joy FM
28 May 2025, 12:18

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa ukisumbumbua katika mataifa mbalimbali kusini mwa jangwa la Sahara.
Na Josephine Kiravu
Zaidi ya vyandarau million 1.7 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 35 vinatarajiwa kusambazwa kwa wananchi Mkoani Kigoma kwa lengo la kupunguza kiwango cha Malaria kutoka assilimia 13%ya sasa hadi kufikia wastani wa Kitaifa ambao ni aslimia 8% ama chini ya wastani huo.
Malaria ni ugonjwa unaozuilika na unaotibika, hata hivyo kila mwaka malaria huwakumba zaidi ya watu milioni 200 na kuua zaidi ya watu laki 600,000 ,na vifo vingi kati ya hivi karibu nusu milioni miomgoni mwao ni watoto wadogo katika bara la Afrika.

Katika kukabiliana na tatizo hilo, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amezindua zoezi la usambazaji wa vyandarau zaidi ya million moja laki saba ambapo amesisitiza matumizi sahihi ya vyandarua hivyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ugavi kutoka MSD Victor Sungusia amesema watahakikisha kaya zote zilizoandikishwa zinafikiwa na kupatiwa vyandarua.
Na hapa wananchi wanatoa shukrani zao kwa Serikali huku wanaume wakihamasisha wenzao kutumia chandarua na kwamba si kweli kama vinapunguza nguvu za kiume.
Zoezi la usambazaji wa vyandarua vyenye dawa ambalo limezinduliwa hii leo linatarajiwa kufikia tamati Juni mosi mwaka huu huku Kauli mbiu ya siku ya Malaria kwa mwaka huu ni Malaria inatokomezwa na sisi,wekeza chukua hatua-Zero malaria inaanza na mimi.
