Joy FM

FAO yataka wanaume kushiriki maandalizi ya lishe kwa watoto

9 May 2025, 16:54

Ni muonekano wa vyakula mbalimbali wakati FAO ikionyesha vyakula vinavyoweza kutumiwa katika lishe bora, Picha na Michael Mpunije

Jamii Mkoani Kigoma imetakiwa kuzingatia suala la lishe bora kwa watoto.

Na Michael Mpunije

Shirika la umoja wa mataifa la Chakula na Kilimo FAO limetoa wito kwa wanaume mkoani Kigoma kushirikiana na wenza wao katika kufanya maandalizi ya chakula ili kuimalisha hali ya lishe kwa watoto katika kukabiliana na utapiamlo.

Shirika la umoja wa mataifa la chakula na Kilimo FAO linasherehekea miaka 80 tangu kuanzishwa kwake Oktoba 16 mwaka 1945 katika mji wa Quebec nchini kanada likilenga kuboresha uzalishaji na ugawaji wa mazao na vyakula kwa na kuboresha hali ya lishe ya watu kote ulimwenguni.

Kupitia programu ya pamoja ya Kigoma (KJP İİ) Afisa lishe Anayefanya kazi shirika la FAO Stella kimambo ametoa wito kwa wanaume kushirikiana na wenza wao katika maandalizi ya chakula ili kukabiliana na udumavu kwa watoto na kueleza kuwa zaidi ya wanufaika 200 kutoka katika halmashauri za Kasulu,Buhigwe na Uvinza wanataraji kunufaika na mafunzo ya lishe.

Sauti ya Afisa lishe Anayefanya kazi shirika la FAO Stella kimambo
Ni muonekano wa vyakula mbalimbali wakati FAO ikionyesha vyakula vinavyoweza kutumiwa katika lishe bora, Picha na Michael Mpunije

Kwa upande wa halamashauri ya mji Kasulu, Afisa lishe katika halmashauri hiyo Bw. John Sabatele amesema bado ipo changamoto kwa jamii ya unene uliokithiri kutokana na baadhi yao kushindwa kuzingatia ulaji unaofaa pamoja na ukosefu wa lishe bora.

Sauti ya Afisa lishe katika halmashauri hiyo Bw. John Sabatele

Baadhi ya wanaufaika wa mafunzo hayo wanaitazama elimu hii kama mwangaza muhimu wakubadili mtindo wa maisha wa kuhakikisha wanazingatia makundi yote 6 ya vyakula kwa kushirikiana na familia katika kukabiliana na udumavu kwa watoto.

Sauti ya Baadhi ya wanaufaika wa mafunzo hayo wanaitazama elimu hii kama mwangaza muhimu wakubadili mtindo wa maisha

Leonard Ofori na leokodia Gajo ni baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo.

Akina mama wakisikiliza elimu ya lishe kutoka kwa ofisa kutoka Fao, Picha na Michael Mpunije