Joy FM
Joy FM
9 May 2025, 10:45

“misingi inayoendelea kuwekwa na chama cha chadema ni misingi inayorudisha uhai wa chama hicho kwa asilimia kubwa”
Na Mwandishi wetu
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wilayani kasulu kupitia Kikao cha baraza la mashauriano ambacho kimeshirikisha viongozi mbali mbali wa chama wameazimia kuwachukulia hatua wanachama na viongozi wote wilayani humo watakao kisalti chama juu ya agenda yao ya kudai mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi .
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kasulu ambaye pia ni diwani wa kata ya mrusi Bw. Fanuel Kisabo pamoja na diwani wa kata ya Nyakitonto Bw, Daniel Nzababa wamesema wataendelea kusimama na chama ili kuhakikisha wanasongambele katika kudai tume huru ya uchaguzi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema jimbo la kasulu Mjini Bw, Idd Jafari pamoja na katibu wa chama wilayani humo Bw, Emmanuel Simon wamewaomba wananchi na wanachama wa chama hicho kuwa wamoja katika kudai mifumo bora ya uchaguzi.
Aidha mwenyekiti wa baraza la wazee wa chama hicho wilayani humo Bw, Gidion Mayani ameiomba serikali kumuachia Mwenyekiti wa chama cha chadema Taifa Tundulisu ili aendelee kukisimamia chama katika malengo mbali mbali waliyojiwekea.
Hata hivyo baadhi ya wanachama ambao wameshiriki kikao hicho wamesema misingi inayoendelea kuwekwa na chama cha chadema ni misingi inayorudisha uhai wa chama hicho kwa asilimia kubwa.
