Joy FM
Joy FM
29 April 2025, 14:54

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na mashirik mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za elimu Mkoani Kigoma.
Na Sadiki Kibwana
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Mohammed Chuachua amegawa vifaa vya sayansi kwa shule za sekondari Mkoa wa Kigoma vyenye thamani ya zaidi ya shilling bilioni 1.2 ikiwa ni katika mpango wa serikali kuinua taaluma nchini.
Hayo yamejili katika ofisi za mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Mkuu wa Wilaya Kigoma ambapo amekabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Tobias Andengenye vilivyotolewa na shirika la UNICEF.
Amesema serikali imejenga miundombinu ya madarasa hivyo wadau kutoa msaada wa vifaa hivyo ni faida kubwa kwa watoto waliopo shuleni.
Aidha Afisa Elimu kutoka UNICEF Mkoa wa Kigoma Farida Sebalua amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwezesha watoto kupenda masomo ya sayansi hivyo itaisaida kukuza masomo hayo.
Baadhi ya Waalimu wa Shule za Sekondari waliokabidhiwa vifaa hivyo kwa Wilaya ya Kigoma wamekuwa na haya ya kusema.
