Joy FM
Joy FM
28 April 2025, 14:56

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha tatizo la utapiamlo linaisha kwa watoto.
Na Josephine Kiravu
Watoto wenye umri chini miaka 5 wapatao 14 ambao wamegundulika kuwa na utapiamlo wamepatiwa dawa lishe ikiwemo maziwa na karanga vyenye thamani ya shilingi million 1.8 kwa ajili ya kuboresha afya zao.

Utapiamlo ni hali ambayo hutokana na kupata chakula ambacho virutubishi vyake havitoshi au viko vingi hadi kusababisha matatizo upande wa afya
Hata hivyo unaweza kuutibu hata kama hauna rasilimali nyingi kwa kumpatia mgonjwa vyakula vingi zaidi na vyenye ubora unaostahili kilishe.
Naye Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mganga Mkuu Manispaa ya Kigoma ujiji, Hashim Mvogogo amewahimiza wazazi kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha wanawapatia lishe bora huku akieleza pia namna wanavyowasaidia watoto waliogundulika kuwa na utapiamlo.
Akiwa katika maadhimisho ya siku ya malaria kwa niaba ya mkuu wa wilaya Kigoma, Afisa tawala wilaya ya Kigoma Dorah Buzaile ametumia wasaa huo kuwahimiza wazazi hasa jinsia ya kike kuwa karibu na watoto wao sambamba na kuzingatia lishe ili kuwalinda watoto dhidi ya udumavu.
Na hapa mmoja wa wazazi ambae anazingatia lishe bora kwa watoto wake anaeleza faida pamoja na urahisi wa kupata lishe bora kwa watoto.