Joy FM

UNIDO yahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia

14 April 2025, 13:49

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza na viongozi kutoka Shirika la Maendeleo ya viwanda la umoja wa Mataifa UNIDO, Picha na Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhamasisha jamii kutumia nishati safi ya kupikia.

Na Josephine Kiravu

Wadau mkoani kigoma wametakiwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kuanzia shuleni hadi majumbani ili kuendelea kupunguza athari za kiafya zitokanazo na matumizi ya kuni na mkaa.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishana Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amesema hayo wakati akizungumza na viongozi kutoka Shirika la Maendeleo ya viwanda la umoja wa Mataifa UNIDO akiwemo Bi Lilian Nyaki na amewapongeza kwa kuyagusa makundi mbalimbali ikiwemo mama lishe na baba lishe pamoja na mashuleni.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishana Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Ameongeza kuwa upatikanaji wa huduma ya umeme umeboreshwa hivyo ni rahisi kwa kila mwananchi kutumia nishati hiyo kwa kupikia kwani inasiaidia pia kupika chakula kwenye mazingira yaliyo safi.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishana Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye

Akizungumza wakati wa kuwasilisha mradi Bi. Lilian Nyaki kutoka Shirika la maendeleo ya viwanda la umoja wa mataifa amesema mradi huo unalenga kuwafikia makundi yote ikiwemo shuleni.

Sauti ya Bi. Lilian Nyaki kutoka Shirika la maendeleo ya viwanda la umoja wa mataifa

Nao baadhi ya mama lishe na Baba Lishe katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wamesema awali gunia moja la mkaa lilitumika kwa muda wa siku tatu huku pia wakihatarisha usalama wa maisha yao kutokana na nishati walizotumia.

Sauti ya baadhi ya mama lishe na Baba Lishe katika Manispaa ya Kigoma Ujiji

Dhima ya mkakati wa Kitaifa wa miaka 10 imelenga kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia iliyo nafuu, endelevu salama na rahisi kutumika.