Joy FM
Joy FM
11 April 2025, 17:28

Wasariamali na wafanyabiashara wadogo wamepewa mafunzo yanayolenga kuwainua kiuchumi
Na Michael Mpunije
Wasimamizi wa taasisi za kifedha wametakiwa kushirikiana na wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati katika kuandaa mpango wa Biashara ili kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.
Hayo yamejiri wakati wa kuhitimisha mafunzo yaliyodumu kwa 6 mjini Kasulu ambayo yamefadhiliwa na shirika la kazi duniani ILO kwa ushirikiano wa serikali ya Norway na Ireland Chini ya mradi wa kigoma pamoja ambao unalenga kuwanufaisha vijana, wanawake na Wakulima wadogo mkoani Kigoma.

Akizungumza na kituo hiki Mratibu wa mradi wa Kigoma pamoja kutoka shirika la kazi Duniani Nureen Toroka ameeleza malengo ya kutoa mafunzo.
Aidha Ameongeza kuwa wataendelea kuwajenga uwezo wasimamizi wa taasisi hizo kuhakikisha wanatoa elimu kwa wajasiriamali kurasimisha biashara zao pamoja na kufanya kazi yenye staha.
Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo akiwemo Thobias Mkamate kutoka NMB foundation kanda ya kati na Kitambala Guka kutoka CRDB Foundation kanda ya Pwani wameeleza namna watakavyotoa mafunzo kwa wafanyabiashara waweze kupata ujuzi wa kuandaa mpango wa biashara katika kukuza uchumi wake.