Joy FM

Maafisa usafirishaji majini watakiwa kuwa na leseni

9 April 2025, 11:34

Pichani ni viongozi wa TASAC wakiwa na wadau wa usafirishaji baada ya kikao kazi kilichowakutanisha na wadao wote wa usafirishaji wa majini mkoani Kigoma,- picha na Sadick Kibwana

Shughuli za usafirishaji kwa njia za maji ni miongoni mwa vyanzo vya mapato kwa taifa la Tanzania pia kwa mwnanchi mmoja mmoja hivyo weledi na ufanisi utafanikisha shughuli hiyo

Na Sadick Kibwana

Wadau wa usafirishaji wa majini Mkoa wa Kigoma hasa mawakala wa Forodha wametakiwa kushughulikia mapungufu yanayojitokeza katika kazi hiyo ili kuhakikisha wanatumia uweledi katika kufanikisha kazi zao ikiwemo kukata leseni kwaajili ya biashara.

Rai hiyo imetolewa katika kikao kazi cha Wadau wa usafirishaji wa majini Mkoa wa Kigoma kiilicho andaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Ambapo Afisa Mdhibiti TASAC Selina Mokiti ambaye alikuwa mtoa mada katika kikao hicho amesema kuna muhimu wadau kutumia weledi katika kazi zao jambo litakalo nufaisha wao na serikali.

Sauti ya Afisa mdhibiti TASAC Selina Mokiti

Aidha Afisa Mkuu Udhibiti, Usafirishaji kwa njia ya Maji TASAC Sylvester Kanyika amesema ni jukumu lao tembelea wadau wao mara kwa mara ili kujua namna gani ya kutatua changamoto zinazojitokeza nchi nzima.

Sauti ya Afisa Mkuu Udhibiti TASAC

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Mkoa wa Kigoma Bwana Abdulrahman Kaponta amesema TASAC wamefanya jambo zuri la kuwakumbusha wadau wao ili kuhakikisha ufanisi unakuwepo kazini.

Sauti ya Mwakilishi kutoka TPA Kigoma

Nae Mwenyekiti wa Mawakala wa Forodha TAFFA Hussein Haruna Kinga amesema kuna changamoto nyingi pia ameomba ushririkiano na wadau wakuu wa Bandari.

 Sauti ya Mwenyekiti TAFFA Hussein Haruna

Wadau wa usafirishaji majini katika kikao kazi na shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC