Joy FM
Joy FM
7 April 2025, 17:01

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Kazi Maalum, Kapteni Mstaafu George Mkuchika akiwa katika ujenzi wa mradi wa kituo cha afya Makere ameeleza kuwa dhima ya serikali ni kuhakikisha wanaimarisha huduma za afya.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Makere halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2 kwa lengo la kusogeza karibu na wananchi kupata huduma za afya
Akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo Meneja wa TANROAD Mkoa wa Kigoma Injini Narcis Choma amesema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 43 ya utekelezaji.
Amesema mradi huo unatekelezwa ikiwa ni mradi wa Nyongeza kutoka mradi mkuu wa barabara ya Kabingo – manyovu wilayani Buhigwe wenye urefu wa zaidi ya kilomita 200.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Kazi Maalum, Kapteni Mstaafu George Mkuchika akiwa katika ujenzi wa mradi huo ameeleza dhima ya serikali kuhakikisha wanaimarisha huduma za afya pamoja na kuongeza watoa huduma za afya ili kuhakikisha wananchi wanaondokan na adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.
Baadhi ya wananchi kata ya makere halmashauri ya wilaya ya Kasulu wameelezea furaha yao endapo mradi huo utakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.