Joy FM

Zaidi ya bilioni 19 zatumika utekelezaji wa miundombinu ya barabara Kasulu

25 March 2025, 14:32

Mkuu wa wilaya Kasul Kanali Isac Mwakisu akizungumza katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM, Picha na Hagai Ruyagila

Serikali kupitia TARURA imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji baada ya kupokea fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Na Hagai Ruyagila

Zaidi ya shilingi bilioni 19 zimetolewa na serikali kupitia kwa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kuanzia mwaka 2020 hadi kufikia mwezi februari 2025 kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM katika kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho wilaya ya Kasulu Mkuu wa wilaya ya hiyo Kanali Isaac Mwakisu amesema miundombinu ya barabara imeendelea kutekelezwa katika halmashauri za Kasulu vijini na kasulu mjini.

Amesema lengo ni kuandoa changamoto ya ubovu wa miundombinu hiyo pamoja na kuweka mawasiliano ya barabara katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kasulu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu
Wanachama wa CCM wakiwa katika kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu Bw.Mbelwa Chidebwe ameimpongeza serikali kwa kutelekeza ilani ya chama hicho katika kujali na kutatua changamoto za wananchi kwa wakati.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu Bw.Mbelwa Chidebwe

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu licha ya kupongeza kwa hatua ya hiyo pia  wamekuwa na maoni tofauti kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Sauti ya Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kasulu