

25 March 2025, 13:01
November 24 mwaka 2021 aliyekuwa waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako alitangaza kuruhusiwa kurejea shuleni kwa wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito kurejea shuleni kwa mfumo rasmi baada ya kujifungua.
Na Josephine Kiravu
Wanafunzi katika kituo cha elimu ya watu wazima Burega katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameiomba Serikali kuona haja ya kuwajengea chumba maalum kwa ajili ya kuwaacha watoto wao muda wa masomo na kuondoa adha wanayokutana nayo hivi sasa licha ya kuahidi kufanya nyema kwenye masomo yao.
Hata hivyo mpaka sasa Serikali mkoani Kigoma imeanza mchakato wa kujenga vyumba maalumu kwa ajili ya wanafunzi waliojifungua kuwaweka watoto wao wakati wanaendelea na masomo kwenye vituo vyao ili iwe rahisi kupata uangalizi kutoka kwa wataalam ambao watawekwa kwenye maeneo hayo.
Ukisikiliza simulizi ya mabinti hawa ambao walikatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito utaungana na ule msemo kwamba kuteleza sio kuanguka kwani matarajio yao ni kufika mbali kielimu na kutimiza ndoto zao walizokatiza hapo awali.
Sauti za wanafunzi.
Na hapa Mwalimu Samson Mabula ambae ni mkufunzi mkazi katika kituo cha Burega anaeleza lengo la Serikali katika kuhakikisha wanafunzi ambao watoto wao hawana uangalizi wanapata uangalizi wa kutosha.
Sauti ya Mkufunzi
Lakini je mpango wa serikali ni upi katika kuhakikisha wanafunzi hao wanatimiza malengo yao?
Sauti ya mkufunzi
Novemba 11 mwaka jana Mkuu wa mkoa Kigoma alizindua kampeni ya kuwaandikisha na kuwarejesha shuleni watotowalio nje ya mfumo rasmi huku akitoa msisitizo kwa wazazi na walezi kushirikiana na viongozi na wasimamizi wa masuala ya kitaaluma ili kudhibiti utoro, na kuhimiza nidhamu chanya na utoaji wa msaada kisaikolojia kwa watoto wanaosoma pale wanapokutana na changamoto za kimaisha.