

17 March 2025, 13:17
Kukamilika kwa ujenzi mradi wa reli ya kisasa SGR kwa kipande cha Tabora-Kigoma unatarajiwa kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi na kufungua shughuli za usafirishaji
Na Tryphone Odace
Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji na mitaji ya umma PIC imetembelea ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Tabora -Kigoma na kumtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuhakikisha anazingatia ubora na viwango vinavyotakiwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji na mitaji ya umma (PIC) Vuma Hole amesema hayo mara baada ya Kamati hiyo kukagua ujenzi wa mradi huo na kuridhishwa na hatua za awali za ujenzi wa mradi huo na kuwa utasaidia wananchi wa Mkoa wa Kigoma na nchi jirani za Congo na Burundi katika shughuli za usafirishaji wa mizigo.
Amesema pia tayari maeneo muhimu yameshajengwa ikiwemo daraja katika eneo la mto malagarasi na kuipongeza Serikali Kwa uamzi wake wa kuendeleza ujenzi wa SGR katika kipande hicho mradi ambao hadi kukamilika kwake utakuwa utagharimu zaidi ya shilingi trilioni moja na kuwa kichocheo cha uchumi.
Sauti ya Mwenyekiti PIC Vuma Hole
Aidha Bw. Vuma amesema Serikali itaendelea kutoa fedha ili kuhakikisha mradi huo unakamilika Kwa wakati na kupunguza gharama za usafirishaji Kwa wananchi wanaotegemea reli hiyo.
Sauti ya Mwenyekiti PIC
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya shirika la reli TRC Ally Karavina amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha ujenzi wa reli hiyo unafanyika kwa haraka na ufanisi ili kusaidia bandari ya Dar es Salaam kupata mizigo ya kudumu na kuufanya bandari hiyo kuwa na mizigo ya uhakika kutoka nchi za Congo na Burundi.
Sauti ya Mwenyekiti wa bodi TRC Ally Karavina
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha reli hiyo inajengwa ili iwe imara na kutoa huduma Kwa muda mrefu na kuwa tayari Kwa kipande cha Tabora Kigoma wananchi wameonyesha kuufurahia mradi huo.