

14 March 2025, 16:43
Mkoani Kigoma Serikali imeendelea kutoa elimu pamoja na kupambana na kudhibiti ugonjwa wa maralia
Na Lucas Hoha
Vyandarua zaidi ya laki moja na thelathini vinatarajiwa kugawiwa bure kwa wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa lengo lakudhibiti na kupambana na ugonjwa wa maralia ambao wa kiwango kikubwa umekuwa ukisababisha vifo kwa akina Mama wajawazito na Watoto wenye umri chini ya miaka 5.
Hayo yamebainishwa kwenye kikao cha utoaji elimu kwa wajumbe wa kamati ya usalama, wakuu wa Idara na wataalamu wa Afya ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma DKT Rashird Chuachua amewataka wananchi kutumia vyandarua watakavyopatiwa kikamilifu na kuepuka matumizi yasiyo sahihi.
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma
Naye Katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota amekemea imani potofu waliyonayo baadhi ya wananchi kuwa matumizi ya vyandarua yanamadhara kwa binadamu ikiwemo kupunguza nguvu za kiume
Sauti ya Katibu tawala wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wamekuwa na maoni tofautitofauti kuhusu vyandarua hivyo kama wanavyosema.
Sauti za wananchi
Kwa mjibu wa Taarifa ambayo imetolewa na mratibu wa ugonjwa wa maralia wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dr Shaban Magorwa amesema kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa maralia katika Manispaa hiyo ni asilimia 8