

14 March 2025, 12:23
Halmashauri ya wilaya ya Kasulu inatarajia kupokea vyandarua vyenye dawa bila malipo zaidi ya laki 3 kwa wananchi watakao jiandikisha
Na Hagai Ruyagila
Watendaji wa kata halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa katika halmashauri hiyo vyandarua ambavyo vinatarajiwa kutolewa na serikali katika halmashauri hiyo.
Mwakilishi kutoka wizara ya afya mpango wa taifa wa kudhibiti Malaria Peter vitanya (NMCP)amebainisha hayo wakati akitoa elimu maalumu kwenye kikao cha uhamasishaji wa kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa kwenye kaya kwa mkoa wa Kigoma.
Amesema ugawaji wa vyandarua bila malipo unatarajiwa katika halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma ili kuhakikisha jamii inakuwa salama na kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Sauti ya Peter Vitanya mwakilishi wa kutoka wizara ya afya
Kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw.Komesha kaminyoge amesema halmashauri inatarajia kupokea zaidi ya vyandarua laki 3 na vitatolewa kwa wananchi watakao jiandikisha huku akisisitiza matumizi sahihi ya vyandarua hivyo.
Sauti ya Kaimu mkurugenzi Kasulu DC
Hata hivyo mratibu wa malaria katika halmashauri hiyo Berlino Mlange amesema halmashauri ya wilaya ya kasulu imefikia asilimia 37 ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria huku mkoa wa Kigoma ukiwa ni asilimia 13 za maambuzi ya ugonjwa huo hivyo ameeleza kuwa wanaendelea kuweka mikakati kuhakikisha kila kaya inapata chandarua ili kukabiliana kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria