

11 March 2025, 15:11
Uhamasishaji na utoaji elimu endelevu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ni muhimu katika utekelezaji mpango wa serikali kwa mtanzania kutumia nishati hiyo ifikapo 2034
Na Hagai Ruyagila
Serikali kuu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA imetoa majiko banifu 352 kwa walengwa wanufaika wa TASAF wa halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma hii ni kutekeleza mpango wa serikali wa asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
Hayo yamebainishwa na Dkt. Joseph Sambali Mtaalam Jinsia na Nishati Vijijini REA kutoka Jijini Dododma wakati waugawaji majiko banifu kwa walengwa wanufaika wa TASAF halmashauri ya Mji Kasulu
Dkt. Sambali amesema serikali imetoa majiko hayo ikiwa ni mpago wa serikali wa miaka kumi ulioanza mnamo mwaka 2024 mpaka 2034 ambao utasaidia jamii kwa kiasi kikubwa katika suala la utunzaji wa mazingira, afya ya binadamu na kuepusha vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Sauti y Dr Joseph Sambali Mtaalamu wa jinsia na nishati REA
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa ugawaji wa majiko hayo amesema serikali imeendelea kuwajali wananchi wake kwa kuwapatia majiko hayo katika uandaaji wa chakula.
Sauti ya Profesa Joyce Ndalichako Mbunge wa Kasulu Mjini
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Mh. Noel Hanura ameishukuru serikali kwa kuwapa majiko hayo wanufaika hao wa TASAF kwasababu yanatumia kuni kidogo pamoja na mkaa kidogo.
Sauti ya mwenyekiti halmashauri ya Kasulu mji Mh. Noel Hanura
Nao baadhi yao walengwa wanufaika wa TASAF waliopewa majiko hayo wameishukuru serikali kwa kupata majiko banifu ambayo yanaenda kuwasaidia katika uandaaji wa haraka wa chakula.
Sauti za Wanufaika wa TASAF