

6 March 2025, 09:40
Waumini wa Dini ya Kikristo Mkoani Kigoma Wametakiwa kumtegemea Mungu pasipo kukata tamaa ili kutimiza malengo yao waliyojiwekea katika maisha yao.
Na, Hagai Ruyagila
Kauli hiyo imetolewa na askofu mkuu wa kanisa la FPCT Tanzania Askofu Steven Mulenga wakati wa hotuba ya Neno la Mungu katika kanisa la FPCT Kasulu Mjini
Askofu Mulenga amesema hutakiwi kukata tamaa licha ya changamoto zinazokukabili bali unatakiwa kumtegemea Mungu ili ufanikiwe katika jambo unalolifanya.
Aidha Askofu Mulenga amesema unapofanya jambo litakalosaidia kukupa maendeleo katika maisha yako wapo maadui wanaoweza kukurudisha nyuma ili usifanikiwe lakini ukimuomba Mungu atakusaidia kuzishinda changamoto hizo.
Kwa upande wao baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo wamesema ni vizuri kumtengemea Mungu maana changamoto ni nyingi na endapo kama hutamtegemea Mungu huwezi kupata mafanikio yatakayo kusaidia katika maisha yao.