Joy FM

Dkt. Mpango mgeni rasmi kongamano la wanawake Kigoma

3 March 2025, 12:13

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akikagua bidhaa mbaliimbali mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa NSSF uliopo mjini Kigoma, Picha na Hamis Ntelekwa

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walioandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.

Na Lucas Hoha

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikagua mabanda ya bidhaa mbaliimbali mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa NSSF uliopo mjini Kigoma katika kongamano la siku ya wanawake.

Katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wa serikali na chama wamehudhuria huku maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake zikiwa zinaendelea kuonyeshwa.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akikagua bidhaa mbaliimbali mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa NSSF uliopo mjini Kigoma, Picha na Hamis Ntelekwa

Kongamano hilo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo iatarajiwa kuadhimishwa kimkoa katika wilaya ya Kibondo Mkoani hukukitaifa ikitarajiwa kufanyika Mkoani Arusha na Rais Dk. Samia Suluhu atakuwa mgeni rasmi.