

27 February 2025, 16:41
Serikali imeendelea kufikisha huduma kwa wananchi kwa kujenga miradi ya mbalimbali ya maendeleo ili kusaidia wananchi kupata huduma za uhakika.
Na Hagai Ruyagila
Kamati ya siasa CCM mkoa wa Kigoma imefanya ziara ya kutembelea miradi minne ya maendeleo katika halmashauri ya mji Kasulu licha ya kupongeza kwa hatua inayoendelea nayo imeagiza ikamilike kwa wakati uliokusudiwa.
Ziara hiyo imeongozwa na katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Christopher Palanjo ambaye amesisitiza miradi yote inayotekelezwa na serikali kuhakikisha inakamilika kwa ukamilifu mkubwa uliokusudiwa ili iweze kuwasaidi wananchi.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye amesema amepokea maelekezo na pongezi zote zilizotolewa na Kamati ya siasa mkoa huku akibainisha kuzifanyia kazi changamoto zote ili miradi yote iweze kukamilika kwa wakati.
Awali akizungumza, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe licha ya kuishukuru serikali amesema wanashirikiana vyema na serikali ili kuhakikisha miradi yote inayoekelezwa na serikali ya awamu ya sita inakamilika kwa ubora.
Miradi iliyotembelewa katika halmashauri ya mji Kasulu ni Ujenzi wa shule ya msingi Kanazi, mradi wa maji wa miji 28, ujenzi wa shedi nane zenye vizimba 176 vya wafanyabiashara katika soko la mnadani, mradi wa ukarabati mkubwa wa hospitali ya halmashauri ya mji Kasulu,