Joy FM

Serikali yaanza kulipa fidia wananchi wanaoishi kando na hifadhi ya Mahale Uvinza

26 February 2025, 16:33

Muonekano wa milima katika hifadhi ya mahale iliyopo wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, Picha na Mtandao

Ili kukabiliana na uharibifu wa misitu na wanyama pori kutoweka serikali imeanza kuwalipa fadia wananchi ili waondoke katika vijiji vilivyopo karibu na milima ya hifahdi ya mahale.

Na James Jovin

Serikali imeanza kulipa fidia na kuhamisha kaya zaidi ya 300 za wananchi wanaoishi kando kando ya milima ya hifadhi ya wanyamapori mahale ikiwa ni mikakati ya serikali kuongeza nguvu ya kulinda mnyama adimu duniani aina ya sokwemtu anayepatikana katika hifadhi hiyo na akiwa katika hatari ya kutoweka. 

Waliofanyiwa tathimini ni wananchi wakazi wa vitongoji vya mahasa na kabukuyungu kijiji cha kalilani ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja zimeanza kutolewa kama fidia kwa wananchi hao kuhamishwa katika vitongoji hivyo na kupelekwa katika maeneo mengine yaliyotengwa na serikali kama anavyobainisha kaimu mkuu wa hifadhi ya taifa ya milima ya mahale halid mngofi

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya uvinza dinnah mathamani na mkuu wa mkoa wa kigoma thobias andengenye wameeleza mikakati ya serikali huku mwenyekiti wa ccm mkoa wa kigoma jamali tamimu akiwatoa wasi wasi wananchi wachache ambao bado wanagoma kuondoka eneo hilo.

Muonekano wa Milima katika hifadhi ya Mahale Uvinza, Picha na Mtandao

Nao baadhi ya wananchi wakazi wa vitongoji vya mahasa na kabukuyungu kijiji cha kalilani wanaopaswa kuhama kando kando ya milima ya mahale inayohifadhi sokwe adimu duniani wamesema.

Sauti ya James Jovin akisimulia habari hii ya Serikali kuanza kulipa fidia