

18 February 2025, 17:24
Mawadiwani katika halmashauri ya wilaya Kigoma wametakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato ya halmashauri hiyo.
Na Tryphone Odace
Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma limepitisha rasimu ya bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 36 ambayo ni makadrio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2025-2026.
Kaimu Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya Kigoma Jesca Mmari amesema hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo na kuwa bajeti hiyo imeongezeka kutokana na jitihada mbalimbali ikiwemo uwepo wa vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vimesaidia kuongeza mapato.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Kigoma Jabir Timbako amesema hiyo iliyopishwa ni shirikishi ambayo imebeba vipaumbele vya wananchi wake.
Kwa upande wake, Katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma Mganwa Nzota amewataka madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanaibua vyanzo vipya vya mapato ili kusaidia halmashauri hiyo kutekeleza mirad mbalimbali ya maendeleo.
Baadhi ya madiwani katika halmashauri ya wilaya Kigoma akiwamo Zuber Mafuta diwani wa kata ya ziwani wamesema kwa sasa ukusanyaji wa mapato katika manispaa hiyo umeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita hali ambayo imesababisha miradi mbalimbali kutekelezwa kupitia kupitia mapato ya ndani.