Joy FM

TRA Kigoma yajipanga kuzuia uingizwaji bidhaa za magendo

17 February 2025, 13:45

Pichani ni Mkuu wa wilaya Kigoma Rashid Chuachua akiwa na Maofisa wa TRA na baadhi ya wafanyabiashara katika hafla ya utoaji tuzo, Picha na Mullovan Chepa

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapatao Tanzania TRA imesema itaendelea kushirikiana na wanfanyabiashara kukabiliana na wanaoingiza bidhaa kwa njia za magendo

Na Timotheo Leonard

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, amekemea uingizwaji wa bidhaa nchini kwa njia za magendo akisema hilo linaisababishia serikali upotevu wa mapato na kuathiri pakubwa viwanda vya ndani.

Andengenye amesema hayo kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dk. Rashid Chuachua, kwenye maadhimisho ya shukrani kwa mlipa kodi yaliyokwenda sambamba na utoaji tuzo kwa walipa kodi waliofanya vizuri kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dk. Rashid Chuachua

Akizungumzia tuzo hizo Naibu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA makao makuu Bi. Julieth Nyamolelo,  amesema hatua hiyo inalenga kutambua mchango wa watu na taasisi zinazofanya vizuri katika kutekeleza wajibu wao kikodi kwa maendeleo yaTaifa.

Sauti ya Naibu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA makao makuu Bi. Julieth Nyamolelo

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Kigoma, Meneja wa TRA wa mkoa huo, Beatus Nchota, katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 walifanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 15.48 huku mkoa wa Kigoma ukipangiwa kukusanywa Shilingi Bilioni 35 katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Sauti yaMeneja wa TRA wa mkoa Kigoma, Beatus Nchota,

Kwa upande wake Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Kigoma, imepongeza TRA kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ambapo sasa Wafanyabiashara wanashirikiana vema na TRA katika masula ya kodi.