

17 February 2025, 11:01
Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania, TIRA imeendelea kuhamasisha wamiliki wa vyombo vya moto na wananchi Mkoani Kigoma kukata bima za vyombo vya moto na bima za afya.
Na Lucas Hoha – Kigoma
Wamiliki wa vyombo vya moto wameomba, Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania, TIRA kutoa elimu kuhusu umhimu wa bima na kujua haki zao pindi vyombo vyao vinapopata ajali.
Wameeleza hayo mara baada ya mafunzo ambayo yametolewa na Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania TIRA kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma yanayolenga kuwaelimisha wananchi kujua umhimu wa kuwa na bima.
Wamesema wamiliki wengi wa vyombo vya moto hawana uelewa kuhusu bima na kuwa kuna kila sababu elimu kutolewa kwa kundi hilo.
Naye Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania, TIRA kanda ya Ziwa Tanganyika Kurenje Mbula amesema Bima ni maisha kwani inamsaidia mtu vitu mbalimbali ikiwemo kutoa gharama ya matibabu kwa mtu mwenye Bima pindi anapopata ajali.
Aidha Mbula amesema wananchi wa Mkoa wa Kigoma wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kushiriki inayotolewa Mamlaka hiyo ili wawe na uelewa kuhusu umhimu wa Bima kwani wapo wanaokosa haki zao za Bima kutokana na kuwa na uelewa mdogo.