Joy FM

Wanasiasa waonywa kutotumia siasa kuvunja mikataba ya miradi

11 February 2025, 10:22

Mkuu wa Mkoa Kigoma Thobias Andengenye Picha na tovuti ya Mkoa wa Kigoma

Serikali ya Mkoa wa Kigoma imewataka wanasiasa kutokuwa chanzo cha mikataba ya maendeleo kuvunjwa bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Na Lucas Hoha

Mkuu wa Mkoa wa Kigom Kamishina Jenerali Mstaafu wa jeshi la zimamoto na ukoaji Thobias Andengenye amewataka wanasiasa kuacha kutumia majukwaa ya kisiasa kuvunja mikataba ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo na badala yake warejee kwenye vipengele vya mkataba kwa kufuata utaratibu wa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa mkoani Kigoma Andengenye amesema kitendo cha kumkataa mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa soko la Mwanga na mwalo wa katonga kilichofanywa na kamati ya fedha ya baraza la madiwani hakikufuata utaratibu.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kigom Kamishina Jenerali Mstaafu wa jeshi la zimamoto na ukoaji Thobias Andengenye

Hivi karibu kamati ya fedha ikiongozwa na Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Lupoli ilimkataa mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa soko la mwanga na Mwalo wa katonga kutoka ASABHI CONSTRACTOR COMPANY kwa madai kuwa umeshindwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati.

Sauti ya Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Lupoli

Mradi wa ujenzi wa soko la Mwanga na mwalo wa Katonga ni miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 16 ambayo inatakiwa itekelezwe ndani ya miezi 12 na kwa mjibu wa mkataba miradi hiyo imebakiza miezi 10 ikamilike kama anavyoeleza mkandarasi mjenzi.

Sauti ya Mkandarasi anayetekeleza mradi wa soko na mwalo wa katonga