

7 February 2025, 16:13
Wananchi na Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Kgoma Ujiji Mkoani Kigoma, wamemkataa mkandarasi anayejenga Soko Kuu la Mwanga na Soko la Samaki katika Mwaro wa Katonga, Kwa Madai ya kushidwa kutekeleza mradi kwa wakati, Na kusababisha hasala kwa wafanyabiashara kwa kukosa maeneo ya kufanyia biashara zao.
Na Lucas Hoha
Kamati ya fedha na uongozi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma imekataa na kumtaka mkandarasi wa kampuni ya ASABHI CONSTRACTOR CAMPANY LIMITED kusitisha utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa soko la Mwanga na Mwalo wa katonga yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 16 kutokana na mkandarasi huyo kushindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati.
Ni baadhi ya viongozi wa kamati ya fedha wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo amabaye pia ni Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Naibuha Lupoli wakionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa mradi wa mradi huo.
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Naibuha Lupoli amesema ujenzi wa soko la Mwanga na mwalo wa katonga imebaki miezi 10 iwe imekamilika na mpaka sasa hakuna chochote ambacho kimefanyika.
Naye mwakilishi wa kampuni hiyo iliyopewa tenda ya ujenzi huo amesema kwa mujibu wa mkataba wanatakiwa kutekeleza mradi huo ndani ya miezi 12 na kuwa bado wako ndani ya muda licha ya kuchelewa kuanza.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wamepongeza hatua ya kamati ya fedha kusitisha mkandarasi huyo kutekeleza mradi huo kwani ameshindwa kufanya kazi na hali hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.