

6 February 2025, 11:56
Wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kuwa na desturi kuchangia kwenye maendeleo ya shule ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri na kuongeza ufaulu
Na Emmanuel Kamangu
Jumla ya madawati 210 yenye thamani ya zaidi ya milioni 11 zimetengenezwa na diwani wa kata ya mrusi halmashauri ya mji wa kasulu Bw, Fanuel kisabo na kuzigawa kwa shule sita za msingi za kata hiyo ndani ya miaka mitano.
Akizungumza katika hafla ya kugawa dawati 110 diwani kisabo amesema dawati hizo zinatimiza jumla ya dawati 210 ambazo amezigawa kwa shule sita za msingi za kata ya mrusi toka mwaka 2020 hadi sasa nakuomba wadau wengine wa maendeleo kuendelea kusaidiana kutatua kero ya uhaba wa madawati katika kata hiyo.
Aidha Diwani kisabo amesema ni wakati wa kufanya kila jitihada ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingra rafiki yatakayo wasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.
Kwa upande wao baadhi ya wakuu wa shule za msingi katika kata hiyo mmoja wao akiwa Bi,Pendo Nkuba wakipokea dawati hizo wamesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua kero ya baadhi ya watoto kusoma wakiwa wamekaa chini.
Katika shule sita za msingi za kata ya mrusi kuna jumla ya wanafunzi 7707 huku shule zote hizo zikikabiliwa na upungufu wa madawati 995.