Joy FM

Mfumo wa tehama wasaidia kumaliza mashauri kwa wakati Geita

4 February 2025, 11:47

Jaji mfawidhi wa mahakama kuu masijala ndogo ya Geita mkoani Geita  jaji Kelvin Mhina, Picha na Samwel Masunzu

Mahakama kuu Masjala ndogo ya Geita Mkoani Geita imesema matumizi ya teknolojia imesaidia kuharakisha na kumaliza mashauri kwa wakati

Imeelezwa kuwa matumizi ya mfumo wa tekonojia TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli za kimahakama umesaidia kumaliza mashauri ndani ya wakati na kwa haraka zaidi

Hayo yameelezwa na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu masijala ndogo ya Geita mkoani Geita  jaji Kelvin Mhina kupitia maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria katika uwanja wa Dkt. Samia Suluhu Hassan EPZA Mjini Geita.

Jaji  Mhina amesema katika kipindi cha mwaka 2024 mahakama hiyo imeweza kusikiliza na kumaliza mashauri zaidi ya elfu 8 sawa na aslimia 94.2.

Sauti ya Jaji mfawidhi wa mahakama kuu masijala ndogo ya Geita mkoani Geita  jaji Kelvin Mhina

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema adhima ya serikali ni kuendelea kuboresha mifumo ya utendaji wa shughuli za kimahama ili zifanyike kwa ufanisi zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela, Picha na Samwel Masunzu
Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela