

4 February 2025, 11:26
Serikali katika Halmashauri ya Mji Kasulu imesema kupitia bajeti iliyopitishwa kuweka kipaumbele cha ununuzi wa madawati katika halmashauri hiyo ili kusaidia kupunguza uhaba wa madawati uliopo katika shule mbalimbali.
Na Michael Mpunije
Idara ya Elimu halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma imeiomba halmashauri hiyo Kuweka kipaumbele cha Bajeti ya mapato ya ndani kuboresha miundombinu ya elimu ili kutatua changamoto zilizopo katika baadhi ya shule za msingi na kusaidia kukuza ufaulu kwa wanafunzi.
Wito huo umetolewa na mdhibiti Ubora halmashauri ya Mji Kasulu Bi, Martha Mlimi katika kikao cha kamati ya Ushauri ya wilaya DCC Wakati wakujadili makisio ya Bajeti ya halmashauri ya mji Kasulu kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Bi,Mlimi amesema bado kuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu ikiwemo uhaba wa matundu ya vyoo,Nyumba za waalimu pamoja na uhaba wa madawati hali ambayo husababisha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac Mwakisu amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri pamoja na kuendelea kutatua changamoto ya uhaba wa madawati shuleni.
Aidha kanali Mwakisu ameomba wadau wa elimu kushirikiana na Serikali kutatua baadhi ya changamoto zilizopo Katika shule za msingi na Sekondari wilayani Kasulu.